TPBRC yasimamisha pambano la Mwakinyo

DAR ES SALAAM. KAMISHENI ya ngumi za kulipwa nchini ( TPBRC), imesimamisha pambano la mkanda wa Middle ubingwa wa WBO, kati ya Bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Patrick Allotey kutoka Ghana.

TPBRC wametoa sababu ya kusimamisha pambano hili ambalo lilitarajiwa kufanyika Machi 31, mwaka huu liloandaliwa na kampuni ya Golden Boy Promotion inayosimawa na Shomari Kimbau.

Makamu Mwenyekiti wa TPBRC, Alex Galinoma amesema tume  ya Kudhibiti Masumbwi nchini, inasikitika kutangaza kutoidhinishwa kwa pambano hili  kutokana na uvunjaji wa mikataba na vigezo na masharti kadhaa.

“Kuna vitu vimefanywa na promota, vimeathiri uadilifu na ubora wa tukio, licha ya  kuwakumbusha mara kwa mara na kujaribu kutatua masuala hayo, mwendeshaji ameshindwa kukidhi mahitaji na majukumu muhimu yaliyowekwa na tume,” amesema Mwenyekiti.

Ameeleza kuwa uwasilishaji usiokamilika wa nyaraka zinazohitajika, pamoja na mikataba kamili ya mabondia, rekodi za matibabu, vibali vya tukio, Kutotii majukumu ya kifedha, ikiwa ni pamoja na malipo yaliyosalia yanayohusiana na ada za mabondia, waamuzi na wasimamizi wa masumbwi, ada za kuidhinisha, leseni, na majukumu mengine ya kifedha.

“Ameshindwa kupata ukumbi unaofaa kwa tukio ndani ya muda uliokubaliwa au kuwakilisha, nakala zinazoonyesha kupatikana kwa ukumbi, Ukosefu wa mawasiliano na ushirikiano na umesababisha  kucheleweshwa na kutofahamishana.

TPBRC inasisitiza ahadi yake ya kudumisha viwango vya juu vya weledi, haki, na uadilifu wa  mchezo wa huo, hatuwezi  kuidhinisha tukio hili chini ya hali. Tunasikitishwa na  usumbufu ambao kutoidhinisha kwa tukio,” amesema Galinoma.

Ameongeza kuwa Kamisheni inaendelea kufanya kazi kwa karibu na  kuhakikisha utekelezaji wa mafanikio wa matukio ya ngumi yanazingatia sheria na kanuni za mchezo huo.

“Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na pande zote zinazohusika kutatua masuala na kupanga tena tukio hilo katika tarehe zijazo, Maboresho zaidi yatatolewa mara tu makubaliano mapya yatakapokamilika,” amesema Mwenyekiti huyo.

Galinoma amechukuwa nafasi ya uwenyekiti na Kamisheni hiyo baada ya Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuwaondoa madarakani Chaurembo Palasa na kamati yake yake.

Habari Zifananazo

Back to top button