TPDC kuongeza tija uzalishaji gesi

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), limeanza kukarabati kisima namba moja cha kuzalisha gesi asilia Mnazi Bay, mkoani Mtwara,  ili kuongeza tija katika uzalishaji wa umeme nchini.

Kisima hicho ambacho kwa sasa kinazalisha gesi futi za ujazo milioni 10 kwa siku. kiligundulika mwanzoni mwa mwaka 1982 na kuanza kuzalisha gesi mwaka 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari katika la kisima hicho, ambacho kipo eneo la baharini Mnazi Bay, Meneja wa Uendelezaji na Uzalishaji wa Gesi TPDC, Mhandisi Felix Nanguka suala hilo linafanyika ili kuongeza uzalishaji kutoka futi za ujazo milioni 10 kwa siku  mpaka milioni 17 kwa siku.

“Kisima hiki kwa sasa kina uwezo wa kuzalisha gesi futi za ujazo milioni 10 kwa siku, ambapo tunatarajia kuongeza futi za ujazo milioni 7 na kufikia futi za ujazo milioni 17 kwa siku,” amesema.

Amesema suala la ukarabati wa kisima hicho inatokana na ongezeko la matumizi ya gesi nchini na kuwalazimu shirika hilo kufanya ukarabati katika kisima hicho kuongeza uzalishaji.

Ukarabati wa kisima hicho unafanywa na Kampuni ya Kuzalisha Gesi ya Maurel Prom kwa kuingiza vifaa maalum ndani ya kisima hicho, ili kusaidia kuongeza uzalishaji.

Kwa mujibu wa Felix, zoezi la ukarabati  linatarajiwa kufanyika kwenye visima vingine ili kuongeza njia za kuzalisha gesi nyingi zaidi.

“TPDC kwa kushirikiana na wadau wetu wa utafiti wa mafuta na gesi wana mpango wa kufanya uendelezaji wa vitalu vingine kwa ajili ya kuongeza matumizi ya gesi nchini ambayo kwa sasa yamekuwa makubwa,” amesema.

Kwa mujibu wa takwimu za TPDC, asilimia 84 ya gesi asilia inayozalishwa nchini inatumika kuzalisha umeme, asilimia 15 inatumika viwandani na asilimia moja inatumika nyumbanii na kwenye magari.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button