TPDC: Uzalishaji gesi Mnazi Bay unaendelea

MTWARA; SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) limekanusha taarifa kuwa visima vitano vya kuzalisha gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay Mkoani Mtwara vimekauka na kuacha kuzalisha gesi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea visima hivyo, Mkurungezi Mtendaji wa Shirika hilo Mussa Makame, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba visima vyote vinaendelea na uzalishaji kama kawaida.

“Uzalishaji wa visima vyote vitano hapa hapa (Kitalu cha Mnazi Bay) unaendelea , hakuna tatizo lolote wala hakuna ukweli wowote kwamba kuna kisima kimekauka au visima havitoi gesi sasa hivi,” amesema.

Makame amesema hali ya uzalishaji kwa sasa katika visima vyote vitano unafanyika kiukamilifu.

Habari Zifananazo

Back to top button