TPHPA: Tunachangia kilimo chenye tija

MLIPUKO wa panya, nzige na kweleakwelea hapa nchini umekuwa ukirudisha nyuma jitihada za serikali za kuongeza tija katika uzalishaji, hivyo Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), inahakikisha inadhibiti hilo kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Dk Joseph Ndunguru ameeleza hayo katika viwanja vya maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Advertisement

Amesema hivi sasa Tanzania inazungumzia uchumi wa viwanda ambao ni lazima kuwe na kilimo chenye tija, hivyo mamlaka hiyo inadhibiti mlipuko huo wa panya, nzige, kweleakwelea pamoja magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao.

“Mamlaka inachangia katika uongezaji wa tija, Tanzania inazungumzia uchumi wa viwanda, uchumi wa viwanda ni lazima tuwe na kilimo chenye tija moja ya kitu cha kufanya ni kwa udhibiti sahihi wa usumbufu wa mimea kwa maana ya magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao.

“Lakini kuna aina mbalimbali za visumbufu ikiwepo mlipuko kwa maana ya panya, nzige, kweleakwelea na kwa kufanya hivyo tunaongeza tija katika mazao na tija ikiongezeka tunachangia kwenye ajira lakini kwenye ukuaji wa uchumi na malighafi ya viwanda,” alisema.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *