TPSF yazungumzia operesheni za NEMC

TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imewashauri wafanyabiashara kuweka mazingira bora na salama kwa watumiaji wa huduma zao kwa kufuata sheria zilizopo.

TPSF imeziomba mamlaka husika ikiwemo Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kuendelea kutoa elimu ya jinsi ya kutekeleza maelekezo yaliyopo kwa wafanyabiashara ili wafuate sheria.

Kaimu Mkurugenzi wa TPSF, Raphael Maganga ametoa ushauri huo siku chache baada ya NEMC kufunga biashara 89 za baa na kumbi za starehe jambo lililoathiri biashara hizo.

“Serikali ya Tanzania inasimamia utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ‘Blue Print’ ambayo inalenga kuboresha mazingira na kuondoa vikwazo kwenye biashara. Agizo hili la NEMC linarudisha nyuma jitihada za serikali za kukuza sekta binafsi,”

“Kufungwa kwa biashara 89 kumeathiri mnyororo mzima wa biashara ikiwemo wasanii, viwanda vya vinywaji, chakula, wavuvi, wasafirishaji na wakulima hivyo kupoteza zaidi ya ajira 5000 pamoja na upotevu mkubwa wa mapato kutokana na biashara hizo kufungwa,” amesema Maganga.

Amesema TPSF inafahamu athari ya uchafuzi wa mazingira hasa wa kelel na madhara yake, na inaheshimu mifumo iliyopo inayolinda mazingira, ila utekelezaji wa sheria, na kanuni unafaa kutekelezwa kwa weledi, haki na usawa kwa wote.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x