TRA Katavi yatoa tuzo 16 walipa kodi bora

Katika kuhitimisha wiki ya mlipa kodi, mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi imekabidhi tuzo 16 kwa walipa kodi bora wa mwaka 2021/22.

Akitangaza washindi hao, Afisa elimu Mwandamizi kwa mlipa kodi (TRA) Makao Makuu, Peter Shewiyo ameitangaza kampuni ya Allyen Industries Limited kuwa mshindi wa jumla wa tunzo hizo.

Shewiyo amesema vigezo vilivyotumika kuwapata washindi hao ni kiwango kikubwa alichochingia kama kodi, kulipa kodi stahiki na kwa wakati, kuwasilisha ritani kwa wakati, kutokupatikana na kosa la aina yoyote kwa kipindi husika.

Katika kundi la walipa kodi wakubwa Shewiyo ameitangaza kampuni ya Katavi Mining Company Ltd kuwa mshindi wa kwanza katika kundi hilo ikifuatiwa na kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Company Ltd huku RK General Supplies Company Ltd ikitangazwa mshindi wa tatu.

Aidha vinara katika kundi la walipa kodi wa kati ni MM (2001) Group Ltd, Infinity Oil Co. Ltd na Madema Company Ltd huku kwenye kundi la walipa kodi wadogo wakitajwa Shabir Hassanali Walimohamed, Bernard Masaba Sayi na Abdallah Ally Soud.

Katika hatua nyingine ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Katavi, Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi na kampuni ya Tobacco Lake Tanganyika, zimepewa vyeti kwa kutambua mchango wao katika ukusanyaji wa kodi mkoani humo.

Wiki ya Mlipa Kodi kwa Mkoa wa Katavi imeadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kufanya usafi katika eneo inapojengwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo,kutembelea Hospitali teule ya Mkoa na kugawa zawadi kwa watoto kuanzia umri wa miaka 0-5,kufanya Bonanza lenye michezo mbalimbali ili kuhamasisha wananchi kulipa kodi kwa hiyari na kugawa vyeti kwa walipa kodi bora.

Habari Zifananazo

Back to top button