TRA kuiwekea mkakati Tanga

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA),  inatarajiwa kuufanya Mkoa wa Tanga kuwa wa kimkakati katika ukusanyaji wa mapato nchini

Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mcha Hassan Mcha, wakati wa kikao na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga cha kujadili changamoto zinazowakabili katika ukusanyaji wa mapato.

Amesema kutokana na mkoa huo kufanya vizuri katika ukusanyaji mwaka wa fedha uliopita, wamejipanga kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wafanyabiasha.

“Tumekuja kuongea na wafanyabiashara, ili kuweka mikakati ya pamoja na namna ya kufikia lengo la ukusanyaji kodi Kwa mwaka huu, ikiwemo kuzifanyia kazi changamoto zilizopo,”amesema Kamishna Hassan.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiasha, Mkurungenzi Mtendaji wa kampuni ya kusambaza nguzo za umeme, Badru Masoud, amesema kuwa kikao kinatoa mwanga wa ushirikiano baina ya wafanyabiasha na TRA kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato kwa hiyari.

Habari Zifananazo

Back to top button