TRA yafafanua malengo ukusanyaji mapato

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imesema imejipanga kwa lengo la kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya Sh trilioni 26.7 kwa nchi nzima katika mwaka huu wa fedha 2023-2024.

Hayo yamesemwa leo na kamishina wa walipa kodi wakubwa kutoka mamlaka hiyo, Alfred Mregi wakati wa semina ya walipa kodi wakubwa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

“Sote tunafahamu kuwa Mamlaka ya Mapato ina majukumu makuu matatu ambayo ni kukusanya,kuhasibu na kuwasilisha kodi zote za Serikali.” amesema Mregi.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2022-2023 Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)ilikusanya jumla ya kiasi cha Sh trilioni 24.01 sawa na asilimia 97 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 24.07.

“Pamoja na juhudi kubwa ambazo mamlaka imekua ikizifanya ili kuhakikisha inafikia kiwango cha makusanyo kilichokusudiwa bado kuna mambo mbalimbali ambayo yanasababisha mamlaka kukosa mapato kutokana na baadhi ya watu au taasisi kutokuwa wazelendo katika taifa lao kwa kukwepa kodi kwa makusudi.” amesema Mregi.

Meneja Kodi wa Mgodi wa Geita Gold (GGM) Godvictor Lyimo amesema kuwa biashara ya magendo inaathiri kubwa kwa wananchi kwani bidhaa nyingi zinakuwa hazijakaguliwa ili kukidhi vigezo vya ubora vinavyohitajika pia inadumaza uzalishaji nchini sambamba na kuikosesha serikali mapato.

Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi.

una maoni usisite kutuandikia

Habari Zifananazo

Back to top button