TRA yakusanya Sh tril.12.4 nusu mwaka

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeeleza kuwa katika kipindi cha nusu ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2022/23 kuanzia mwezi Julai 2022 hadi Desemba 2022, imekusanya Shilingi trilioni 12.

46 ikiwa ni sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya Shilingi trilioni 12.48.

Taarifa ya TRA, iliyotolewa Januari 1, 2023 na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Alphayo Kidata imeeleza kuwa makusanyo hayo ni ongezeko la Shilingi trilioni 1.35 ikilinganishwa na kiwango cha makusanyo cha Shilingi trilioni 11.11 kilichokusanywa kwa kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 sawa na ukuaji wa makusanyo wa asilimia 12.2.

“TRA inapenda kuutaarifu umma kuwa katika kipindi cha Desemba 2022 imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 2.77 kati ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 2.60, makusanyo ya mwezi Desemba 2022 yana ufanisi wa asilimia 106.5, sawa na ukuaji wa asilimia 10.

3 ukilinganisha na makusanyo ya mwezi Desemba 2021,” imesema taarifa hiyo.

TRA imesema kuwa pamoja na makusanyo hayo kuvuka lengo la mwezi Desemba 2022, ndicho kiwango cha juu zaidi kukusanywa kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa mamlaka mwaka 1996.

“Tunaendelea kuwashukuru walipa kodi na wadau wetu mbalimbali kwa kujitoa kwenu katika kipindi cha nusu mwaka ambapo mwenendo wa ulipaji kodi kwa hiari na mahusiano baina ya mamlaka na walipakodi umeendelea kuimarika kwa kiwango cha kuridhisha,” imesema.

Habari Zifananazo

Back to top button