TRA yasisitiza tozo ya kitanda nyumba za wageni
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Geita imewataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuzingatia malipo ya tozo ya kitanda kwani ipo kwa mjibu wa sheria.
Hayo yamelezwa Januari 11, 2023 na Ofisa Elimu ya Mlipa Kodi na Huduma kwa Mteja TRA Geita, Justine Katiti alipokuwa akizungumuza na wamiliki wa nyumba wa kulala wageni mjini Geita.
Amefafanua, tozo ya kitanda ni mojawapo ya vyanzo vya mapato ya kuendeleza utalii inayolipwa kutoka malipo ya mgeni kwa usiku mmoja au sehemu ya siku kwenye nyumba ya wageni lililosajiliwa.
Amesema wamiliki wa nyumba za kulala wageni hawapaswi kulalamika kwani inatozwa kwa mjibu wa kifungu cha 59 cha sheria ya utalii ya mwaka 2008 na hivo kila mhusika awajibike.
“Ni lazima muelewe, tozo hii inatozwa kwa asilimia moja tu ya bei ya chumba, na inatozwa kwa kuzingatia bei halisi na siyo bei pungufu ya makubaliano yeyote, baina ya mmiliki na mteja.
”