TRA yawafunda wafanyabiashara Nyang’hwale

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA), mkoani Geita, imewaomba wafanyabiashara wilayani Nyang’hwale kusajili na kurasimisha biashara zao kwa kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), ili kukidhi vigezo vya kupata tenda mbalimbali.

Ofisa Elimu na Huduma kwa mlipa kodi Mkoa wa Geita, Justine Katiti amebainisha hayo  leo, wakati  akizungumuza na wafanyabiashara wa eneo la Busolwa na Kharumwa wilayani  humo.

Amewaeleza wafanyabiashara wanapaswa kujenga utamaduni wa kuweka kumbukumbu ya biashara, kwani kutofanya hivo kunawanyima fursa ya kukopesheka kwenye taasisi za kifedha kwa kukosa taarifa sahihi.

Amesema ili kupata kumbukumbu sahihi za biashara, ni vyema watumie Mashine za Kielektroniki za Risiti (EFD) na kuepuka kufanya makadirio yasiyo sahihi na yenye udanganyifu.

“Kutoa risiti kila bidhaa inayouzwa ni takwa kisheria, tunaendelea kuwakumbusha ukiuza toa risiti na mteja ukinunua dai risiti,” alisema na kuongeza kuwa:

“Tunafahamu changamoto za biashara, ukiona umepata changamoto  tupe taarifa kwa maandishi, ili kuondokana na faini sisizo na tija.”

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x