MAMLAKA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA )Mkoa wa Kagera imeadhimisha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 7 na fedha Sh milioni 1 kituo cha watoto yatima Ntoma kilichopo Bukoba vijijini mkoani Kagera .
Naibu Mkurugenzi wa fedha za makusanyo ya kodi na yasiyo ya kodi, Ramadhan Sengati kutoka TRA wakati akikabidhi msaada huo alisema wameguswa na jambo la kuwanyonyesha watoto linalofanywa na kituo hicho kinachomilikiwa na kanisa la Kiinjili la kiluthel Tanzania (KKKT ).
Sengati alisema mamlaka hiyo kama sehemu ya jamii kupitia wiki maalum ya kumshukuru mlipa kodi huwa wanafanya mambo mengi ikiwemo kupata wahitaji ambao wapo katika mazingira magumu ili waweze kuwachangiwa walichojaliwa hivyo kuchagua kituo cha watoto wadogo cha Ntoma.
‘’Tulichagua kituo hiki cha Ntoma kutokana na kazi kubwa ya walezi ya watoto hao ya mitume na manabii,sisi kama jamii pia tumeguswa na yanayotendeka hapa kituoni “alisema Naibu mkurugenzi wa fedha za makusanyo ya kodi na yasiyo ya kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania.
Alisema msaada uliotelewa ni vyakula ,vinywaji,viburudisho,sabuni,maziwa ya kopo na pampers vyote vinathamani ya Sh milioni 7 na fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 1.
Comments are closed.