TRA yazindua kampeni utoaji risiti EFD

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua kampeni maalumu ya TUWAJIBIKE yenye lengo kuwakumbusha wafanyabiashara wote na watoa huduma kutoa risiti halali za EFD kila wauzapo bidhaa ama kutoa huduma.

Aidha Kampeni hiyo imelenga kuhamasisha wanunuzi wa bidhaa kudai risiti na kuzikagua kujiridhisha kama zinakidhi vigezi muhimu pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofata Sheria katika utoaji wa risti na wanaotoa zisizolingana na thamani halisi ya bidhaa.

Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa Kodi (TRA) Richard Kayombo amesema zoezi hilo litafanywa na Maafisa wa TRA wa ngazi za Mkoa na Wilaya zote ambapo watakaobainika kufanya udanganyifu wowote watachukuliwa hatua ambazo ni faini na kufungiwa.

Advertisement

Ameongeza kuwa baadhi ya biashara ambazo zimekuwa sugu kwa kutotumia mashine hizo ni wasafirishaji wa Vifurushi na Vipeto pamoja na sehemu za burudani ambapo amesisitiza kuwa lazima watumie kwasababu ni takwa la kisheria.

Aidha amesema mfanyabiashara atakayebainika kutotoa risiti halali au kufanya udanganyifu faini ya Sh milioni 3 hadi milioni 4.5 kwa mnunuzi ambaye hatadai risiti ni Sh elfu 30 mpaka milioni moja na nusu.

Amesema kampeni imelenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma kote nchini kuwajibika kudai risiti halali ya EFD pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vyote muhimu.

Amesema wananchi wanaponunua bidhaa wanastahili kudai risiti na kuhakikisha wanaikagua Ili kujiridhisha inakidgi vigezo vinavyotakiwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *