Treni kuchukua mizigo Bandari ya Tanga

TRENI ya mizigo ya shirika la Reli nchini (TRC), imeanza kuingia Bandari ya Tanga kwa ajili ya kubeba mizigo.

Hatua hiyo imechukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA),  kufuatia agizo la Makamu wa Raisi Dk Philip Mpango alilolitoa hivi karibuni, akitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaingia Bandari ya Tanga na kuchukua mizigo.

Meneja wa Bandari ya Tanga, Masoud Mrisha amesema tayari kichwa cha treni kimeingia katika bandari hiyo kwa  ajili ya kuonesha uwezo wa kuvuta behewa mpaka tatu kwa ajili ya kupakia mzigo.

“Agizo hilo tumelifayia kazi na wiki mbili au tatu hapo nyuma nilishuhudia mimi mwenyewe kichwa cha treni kikiingia ndani ya bandari na kuanza kuonesha kitakuwa na uwezo wa kuvuta behewa mpaka tatu kwa ajili kuchukua mizigo,” amesema.

Kufuatia hatua hiyo, Mrisha amewaomba wateja wa Bandari ya Tanga ambao wanataka kusafirisha au kuchukua mizigo kutumia treni wafanye hivyo, kwa kuwa sasa treni inaingia katika bandari hiyo na kuchukua mizigo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Dillon foya
Dillon foya
8 months ago

Tunamshukuru kuwa Miradi ni mingi na yenye kuhitaji fedha nyingi lakini hatutaacha kulia na mtoto akilia ili anyamaze basi unampa chakula ndipo atulie
Mbeya tumeahidiwa barabara njia nne Igawa ,Songwe Hadi Tunduma kwa muda Sasa
Pia Barabara ya Mchepuko kwa ajili ya Magari makubwa kuleta msongamano katikati ya Mji wa Mbeya na kusababisha Ajali Mlima Iwambi/Mbalizi kwa kufeli breki tumepotza roho za wapendwa wetu Barabara ya Inyala Hadi Songwe lini hizi nazo zitatekelezwa jambo hili ni muhimu sana

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x