Trent Anord nje kwa wiki kadhaa

BEKI wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa akiuguza jeraha la goti, meneja msaidizi Pepijn Lijnders amethibitisha.

Trent alikuwa sehemu ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Arsenal Kombe la FA katika uwanja wa Emirates Jumapili.

“Kwahiyo amepasuka kidogo kwenye mshipa wa goti na atahitaji muda kupona, alifanyiwa ‘scan’ na atakuwa nje kwa wiki kadhaa.” Lijnders amesema.

Virgil van Dijk alikosa mechi hiyo kwa sababu ya ugonjwa lakini huenda akarejea tena katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Fulham Uwanja wa Anfield Jumatano.

Habari Zifananazo

Back to top button