Trump atakiwa kujisalimisha
ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump amefunguliwa mashtaka ya ulaghai na msururu wa uhalifu katika uchaguzi mkuu wa 2020 katika nafasi ya urais nchini Marekani.
Takribani miaka miwili sasa uchunguzi umekuwa ukiendelea dhidi ya Trump kubatilisha kushindwa kwake katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya Joe Biden katika jimbo la Georgia nchini Marekani.
Mwendesha mashtaka wa Kaunti ya Fulton Fani Willis aliwaambia waandishi wa habari kwamba Trump amepewa muda hadi Agosti 25 kujisalimisha kwa hiari kwa mamlaka.
Kwa upande wao mawakili wa Trump wamesema “wanatarajia mapitio ya kina ya shtaka hili ambalo bila shaka lina dosari na kinyume cha katiba kama mchakato huu wote ulivyokuwa”.
Itakumbukwa hili ndilo shtaka kubwa zaidi kwa Trump ambaye sasa ni mgombea urais wa chama cha Republican akiwa na miaka 77.
Hata hivyo, kwa sasa anakabiliwa na kesi mjini New York, Washington, DC na Florida katika kesi nyingine tatu.