TSC yapongezwa mfumo kupokea malalamiko
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Angellah Kaiuruki amezindua Mfumo wa Kielektroniki wa Kupokea Malalamiko ya walimu kwa muda mfupi na akapongeza Tume ya Utumishi wa Walimu ( TSC) kwa kuanzisha mfumo huo ambao utakuwa suluhusho la changamoto za walimu ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya watumishi.
Kabla ya kuzindua wa Mfumo huo unaojulikana kama Teacher’s Service Commission Management Information Systems (TSC-MIS) jijini Dodoma kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume, Waziri Kairuki aliipongeza TSC kwa kusimika mfumo huo ambao pamoja na faida nyingine nyingi utapokea na kutatua changamoto za walimu kwa haraka.
“Naipongeza TSC kwa kutatua changamoto za walimu tangu kuanzishs kwake 2016, lakini kwa kusimika mfumo huo itahaharikisha kupokea na kutatua changamoto za walimu popote walipo bila kulazimika kufika ofis za tume,” alisema.
Pia aliwapongeza vijana wa kitanzania watalaamu wa Teknolojia ya Habari (IT) waliojenga mfumo huo wakiwamo watalaamu kutoka OR-Tamisemi, TSC OR-Utumishi na mtandao wa mawasiliano serikalini (e-govt), Chuo cha Mzumbe na Chuo Kikuu cha Sokoine.
Akizungumzia faida za mfumo huo wa Kielektoniki (TSCMIS), Katibu wa TSC, Paulina Nkwama alisema, mfumo huo unaondoa mfumo wa zamani ambao haukutoa taarifa sahihi za walimu, na hazikupatikana kwa wakati na ulitumia gharama nyingi na muda mwingi walimu kufika makao makuu.
“Lengo la mfumo huo ni kuberesha na kurahisisha utendaji kazi wa shughnuli za kila siku katika kuwahudumia walimu na wadau mbalimbali,” alisema Nkwama.
Nkwama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi alisema, mfumo huo unalenga kusaidia walimu kupata hnuduma mbalimbali wakiwa katika vituo vyao vya kazi pamoja na kuwaondolewa usumbufu wa kufuata huduma kwenye ofisi za TSC nchini.
Akizungumzia muundo wa Mfumo huo, Mkuu wa Kitendo cha TEHAMA na Takwimu TSC, Kainda Ndasa alisema, mfumo huo una module sita ikiwemo ya inayohusu nidhamu za walimu, ya rufaa, malalamiko, mafao kwa wastaafu na ya usajili wa walimu, barua za walimu na mikataba ya ajira pamoja na ile ya taarifa za wageni wanaofika ofisini.
Kupitia mtandao huo walimu popote walipo katika vituo vyao kwa kutumia simu zao za viganjani, wanaweza kuwasilisha malalamiko yao kwenye tume na kupatiwa suluhisho kwa haraka na kwa wakati.