Tshabalala kuikosa Raja

Simba kusukwa upya

Simba itamkosa nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca Jumamosi wiki hii nchini Morocco kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza safari ya Morocco leo kikiwa na wachezaji 13, huku wengine tisa wakitarajiwa kuungana na wenzao kesho baada ya kukamilisha majukumu ya timu za Taifa.

Licha ya Tshabalala, wachezaji wengine sita watakaokosekana kutokana na sababu mbalimbali  ni Mohammed Outtara, Jonas Mkude, Augustine Okrah, Jimyson Mwanuke, Ismail Sawadogo na Mohamed Mussa.

Advertisement

Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally ameeleza kuwa mchezo wao dhidi ya Raja Casablanca unataraji kupigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mohamed V na unatarajai kuanza saa 4 usiku kwa saa za Morocco, ambapo kwa Tanzania itakuwa ni saa 7 usiku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *