NAHODHA msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema wamejipanga kuhakikisha kesho wanapata pointi tatu mbele ya watani wao Yanga.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari beki huyo amekiri kwamba wanakwenda kukutana na timu bora lakini maandalizi waliyofanya ni mazuri na wataka kushinda ili kushinda taji la Ligi Kuu.
“Hata sisi bado tupo kwenye mbio za ubingwa na tunajua kwamba huu mchezo kama tutapoteza basi ndio itakuwa hatima yetu sababu watakuwa wametuacha mbali lakini kila mchezaji amepania kuhakikisha tunapambana na kupata pointi tatu,” amesema Tshabalala.
Nahodha huyo amesema hawapo tayari kuona wapinzani wao Yanga, wanatangazia ubingwa mbele yao hivyo wamejipanga kuhakikisha wanapambana hadi dakika ya mwisho kupaa matokeo mazuri.