Tshala Muana afariki dunia

NGULI wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Elizabeth Tshala Muana (64) amefariki dunia jijini Kinshasa alfajiri leo. Chanzo cha kifo cha chake hakijajulikana mpaka sasa.

Taarifa za kifo chake kimethibitishwa na mume wa marehemu, Claude Mashala, kupitia chapisho lake la Facebook.

“Mapema asubuhi ya leo, Bwana mwema alichukua uamuzi wa kumchukua Mama wa Taifa Tshala Muana. Mungu mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa duniani. Kwaheri Mama ,”ameandika Mashala.

Marehemu Tshala Muana alipata umaarufu barani Afrika kwa nyimbo kadhaa Zaidi kupitia nyimbo zake ‘Karibu Yangu’ na ‘Dezo Dezo’.

Habari Zifananazo

Back to top button