Tshisekedi aongoza kura za urais

DR CONGO: TUME ya Uchaguzi ya DR Congo (CENI) imeendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa rais kwa baadhi ya maeneo ambapo kuanzia Desemba 20-21, kiongozi aliye madarakani Félix Tshisekedi anaongoza kwa tofauti kubwa zaidi ya 80% ya kura zote.
Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa ni kwa wapiga kura 1,876,827, kati ya milioni 44 waliosajiliwa katika nchi hiyo yenye wakazi karibu milioni 100.
Mfanyabiashara na gavana wa zamani wa Katanga (Kusini-Mashariki) Moïse Katumbi ana asilimia 15.18% na mpinzani mwingine Martin Fayulu asilimia 1.2%.
Wagombea wengine zaidi ya ishirini katika kinyang’anyiro hicho, akiwemo mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel Denis Mukwege, walishindwa kufikia 1%.
MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button