MKUU wa Wilaya ya Lindi Shaibu Issa Ndemanga amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Meneja Huduma za Habari za Lugha za Kigeni, Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Christopher Majaliwa kuhusu fursa za mbalimbali kimaendeleo na uwekezaji zilizopo katika wilaya hiyo.
Viongozi hao pia wamejadili jinsi uongozi wa |Wilaya pamoja na Halmashauri zake zitakavyoshirikiana na
TSN kuweka mikakati ambayo itawezesha kutangaza fursa hizo za kimaendeleo pamoja na uwekezaji kupitia matoleo maalumu ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali na majukwaa ya kibiashara.
Mbali na kuchapisha magazeti, kampuni ya TSN hutoa huduma za uchapishaji wa biashara na ushauri wa kimedia.