TSN, Vijana connect waunganisha nguvu

KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) imesaini hati ya makubaliano ya kudumu na Taasisi isiyo ya kiserikali ya ‘Vijana Connect’ kwa lengo la kuibua fursa mbalimbali kwa vijana na namna vijana hao wanavyoweza kunufaika na fursa hizo.

Akizungumza leo Machi 16, 2023 katika ofisi za matangazo Samora Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Lamau Mpolo amesema lengo la makubaliano hayo ni kuwajengea vijana uzalendo katika kutumikia fursa mbalimbali ikiwemo za uongozi, kilimo, mazingira na nyinginezo.

Amesema vijana wana wajibu wa kupanga maendeleo ya taifa, hivyo makubaliano hayo yatahakikisha TSN inaibua fursa zilizopo kwa vijana kupitia kandarasi mbalimbali za serikali.

“Lengo letu ni kuanzisha mijadala mbalimbali ya maendeleo, vijana wote wanashiriki kupanga maendeleo ya taifa vijana wana wajibu wa kupanga maendeleo”.amesema Mpolo.

Mwenyekiti wa Vijana Connect, Hamza Jabir amesema lengo la taasisi yao ni kuangalia fursa za kiserikali na siziso za kiserikali kwa lengo moja la kuwapa hamasa na kuwafaidisha vijana kupitia taasisi yao.

Amesema kuna vijana wengi wa maeneo mbalimbali ambao wamekuwa hawafikiwi na upatikanaji wa fursa hasa katika maeneo ya mikoani, hivyo kupitia makubaliano hayo TSN itaweza kuwafikishia vijana wengi fursa hizo.
“Tumekuwa na program mbalimbali kwa vijana nchi nzima, lengo ni kuwafikia vijana na namna gani wanaweza kutumia fursa, wapo vijana wengi ambao tumewafikia na tunaendelea kufanya hivyo”. Amesema Jabir.

Habari Zifananazo

Back to top button