TSN yampokea Boss mpya
DAR ES SALAAM: KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Aisha Dachi amepokelewa ofisini kwa mara ya kwanza leo na Menejimenti ya kampuni hiyo baada ya uteuzi wake kutangazwa jana.
Dachi anakaimu nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake, Tuma Abdallah ambaye amestaafu utumishi wa umma.
Mkurugenzi TSN ateuliwa Mjumbe wa Bodi TBC
Kabla ya uteuzi huo, Dachi alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Redio katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Sasa anatarajiwa kuongoza jahazi la TSN, linalozalisha Magazeti ya Daily News, HabariLEO, SpotiLEO, Sunday News na Televisheni ya Mtandaoni ya Daily News Digital.
View this post on Instagram