TTB yasisitiza wadau kutangaza vivutio vya utalii

BODI ya Utalii Tanzania (TTB), imesisitiza wadau kuungana na serikali katika kuongeza wigo wa watalii nchini pamoja na kutangaza vivutio vilivyopo, ili lengo la watalii milioni tano kufikiwa.

Meneja Masoko wa TTB, Nassoro Garamatatu amesema hayo leo Dar es Salaam, wakati akizungumza katika maandalizi ya safari ya wafanyabiashara kwenda nchini China inayoratibiwa na kampuni ya GNM Cargo kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo Tanzania.

Amesema bado fursa ziko wazi kwa ajili ya kuongeza watalii nchini na kufikia lengo lililopangwa na serikali, hivyo ni vyema wadau kujitokeza ili kufikia fursa hiyo.

Amesema  Bodi iko tayari na ina nia chanya katika kuwakaribisha wadau mbalimbali wenye nia nzuri itakayowezesha kuongezeka kwa watalii nchini, ili kuongeza pato la Taifa lakini pia kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“TTB imekuwa na mkakati wa kutangaza utalii zaidi duniani ukiwemo ule wa michezo na hata wa utamaduni, tunatoa fursa kwa wadau ili wakatangaze vivutio vyetu vilivyoko  nchini,” amesema Garamatatu.

Kuhusu safari ya China amesema  ni jambo linaloleta uhusiano mzuri baina ya serikali n aa wadau na ahata nchi ya China , hivyo ni eneo ambalo litaongeza fursa za kukuza utalii.

Kwa upande wake, Mratibu wa safari, kutoka GNM, Anthony Luvanda amesema mbali ya kampuni hiyo kuwa wasafirishaji wa mizigo kutoka China kwenda Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki, wameamua kuandaa safari kwa wafanyabiashara wasiojua kwa kuanzia kwenda nchini China, lakini pia wakihamasiaha vivutio vya utalii vilivyopo  nchini.

Amesema licha ya Wachina kuingia nchini katika masuala mbalimbali, lakini ni wachache sana wanaoingia nchini kama watalii, hivyo safari hiyo inayotarajiwa kuanza Oktoba 14-20, inalenga kuhamasisha jamii hiyo kuja kuona vivutio vilivyopo nchini.

Amesema wafanyabiashara watakaokwenda wataweza kufanya utalii kwa baadhi ya miji iliyoko nchini humo, huku wakieleza vivutio vya Tanzania, ambapo pia watashiriki katika maonesho makubwa ya biashara ya 133 ya China.

Amesema safari hiyo inatarajiwa kuwa na Watanzania wapatao 100,  na kupitia utaratibu huo wataweza kuwapatia huduma mbalimbali zinazotakiwa kuanzia tiketi, malazi na hata visa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button