TTCL yazindua T – PESA ‘APP’

Kutumika na mitandao mingine si lazima uwe na laini ya TTCL

SHIRIKA la Mawasiliano  Tanzania- (TTCL)  imezindua akaunti ya pepe (Virtual Wallet) kwa wateja wake kuelekea katika ujenzi wa Tanzania ya Kidijitali.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 9, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL Lulu Mkudde amesema Kampuni ya T-PESA ni mdau mkubwa katika kukuza matumizi ya mifumo ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Amesema,  dhamira ya T-PESA ni kuhakikisha inaendelea katika  kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika ujenzi wa Tanzania ya Kidigitali.

“Leo, tunasherehekea ubunifu wa kipekee kabisa kutoka T-PESA wa kufungua akaunti yako kiganjani mwako popote pale ulipo ijulikanayo kama Akaunti Pepe.” Amesema Lulu na kuongeza

“Hii ni suluhisho la matumizi ya huduma za kifedha inayomwezesha kila mmoja wetu, kufurahia huduma za kifedha kidijitali kupitia ubunifu huu mpya kupitia simu janja ya mkononi kuweza kufungua akaunti na kupata huduma za kifedha na zenye uhakika si lazima uwe na laini ya TTCL unaweza kuwa na laini ya mtandao wowote wa simu.”Amesema

Akaunti Pepe hiyo ni  Teknolojia inayoruhusu watanzania kutuma na kupokea pesa kwa urahisi, kulipa bili, na kufanya manunuzi kwa njia ya kidijitali pasi na kuwa na SIMCARD.

“Kupitia Akaunti Pepe utaweza kupata huduma za kifedha zenye uhakika, rahisi na salama, vilevile huduma hii inawezesha kuwa sehemu ya mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.”Amesisitiza Lulu

Kwa upande wa Mkurungenzi Mkuu wa Mamkala ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) Latifah Khamis ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema  amefurahi kusikia huduma hiyo  inaweza kutumiwa na wateja wote hata kutoka mitandao mingine ya simu,

Amesema  uzuri wa huduma sio tu uwe na laini ya TTCL hata wenye mitandao mingine ya simu wanaweza kutumia.

“Jambo hili ni zuri sana kwa kuwa linafungua fursa kwa wananchi wote kutumia huduma hiyo.

“Hii ni suluhisho la matumizi ya huduma za kifedha ambalo linamwezesha kila mmoja wetu, kufurahia huduma za kifedha kidijitali kupitia ubunifu huu mpya na wakipekee kabisa kumwezesha kila mmoja wetu kupitia simu janja yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti yake na kupata huduma za kifedha na zenye uhakika.”Amesema

Amesema, kwa mara ya kwanza, Watanzania wana uwezo wa kujifungulia akaunti zao za kifedha wenyewe kiganjani mwao kupitia simu janja zao, ambayo inawawezesha kufanya shughuli za kifedha kwa urahisi na haraka bila hitaji la kuwa na laini ya simu.

“Haya ni Mapinduzi makubwa na ya kwanza nchini Tanzania katika sekta hii ya kifedha. Uzinduzi huu wa T-PESA, ni hatua kubwa katika kuleta ufanisi, urahisi na uharaka  wa mabadiliko ya kidijitali na kuimarisha sekta ya huduma za kifedha nchini Tanzania popote pale alipo.

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button