Tuchel kuinoa Bayern

IMEELEZWA kuwa Thomas Tuchel huenda akawa kocha mpya wa Bayern Munchen saa kadhaa zijazo kuanzia sasa.

Taarifa ya aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo wa Skysport ambaye maarufu kwa utoaji wa taarifa za michezo, Fabrizio Romano amesema Tuchel ameshasaini mkataba wa miaka miwili na nusu hadi June 2025.

Ameleeza kuwa katika makubaliano ya Tuchel na Bayern, kocha huyo ataanza mazoezi yake ya kwanza Jumatatu akiwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Tuchel aliondoka Chelsea 9 Sept 2022 baada ya uongozi wa timu hiyo kutopendezeshwa na matokeo ya timu hiyo kwa kipindi hicho. Bayern jana ilimfuta kazi kocha wake, Julian Nagelsmann

Habari Zifananazo

Back to top button