Tuchel kurejea PSG?

Klabu ya Paris Saint German inajiandaa kumrejesha kocha Thomas Tuchel.

Kocha huyo alitimuliwa Disemba 2020.

Mtandao wa Evening Standard umeripoti taarifa hiyo baada ya timu hiyo kuona mwenendo mbovu wa kocha wa sasa Chirstophe Galtier.

Licha ya kuongoza katika msimamo wa Ligue 1, PSG imekuwa na mwenendo usioridhisha.

Timu hiyo ilipoteza dhidi ya Bayern Munchen katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya hapo ilipoteza mchezo wa ligi dhidi ya Monaco.

Timu hiyo inaongoza kwa pointi 57 katika msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa ikiwa na pointi 57 ikifuatiwa na Marseille wenye 54.

Habari Zifananazo

Back to top button