Tukadange?

MFANYABIASHARA maarufu wa vipodozi soko la Kariakoo, anayefahamika kwa jina la Sinyagile ‘Sinyaa’ amedai kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawafuata mpaka nyumbani kudai kodi.

Sinyaa ameyasema hayo leo Mei 17, 2023 mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kikao cha wafanyabiashara kinachoendelea katika uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam akilalamikia utitiri wa kodi ikiwemo kero ya fedha za takataka.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, kero kubwa kwetu ni kodi ya takataka, anakuja mtu wa taka dukani unalipa sh 40,000 akitoka hapo  anakuja kuniambia pesa ya taka za  stoo …stoo inazalisha taka Mheshimiwa Waziri Mkuu?

“Tunanyanyasika sana watu wa vipodozi tunakuwa kama mbwa, TRA wanakuja mpaka nyumbani, nyumbani kuna ofisi?” Alihoji na kuongeza

“Wanatutishia eti wata ‘cease’ biashara zetu, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu je tukadange?….ebu tuambie biashara zetu zikifa tukadange?

“Nina mengi naomba namba yako Mheshimiwa Waziri, naomba appointment……nina mengi sana ya kuongea, duka langu limefilisika…..

“Nikipeleka mtu polisi wanasema tumekuzoea….sasa mazoea mkate, nitaenda kwa Waziri mkuuu.”Amesema

 

Habari Zifananazo

Back to top button