‘Tukiacha woga tutazalisha wasanii wengi wazuri’

MWIGIZAJI mkongwe wa filamu Single Mtambalike, ‘Richie’ amewaomba maprodyuza wa filamu kuacha woga wa kutowaamini waongozaji wa kazi zao.

Akizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam, msanii huyo amesema maprodyuza wengi wa bongo hawataki kuwaamini waongozaji wa kazi zao tatizo ndio linapoanzia hapo.

“Mwongozaji ndie anajua nafasi hii inamfaa nani acheze, lakini wewe unampelekea stori na jina la mtu hapa acheze mtu fulani unamnyima nafasi ya yeye kufanya kazi yake.

“Prodyuza usipomuamini muongozaji huwezi kumwamini msanii chipukizi na itasababisha kutokupa vipaji vipya, watabaki wasanii walewale,” amesema na kuongeza:

“Unaweza kumwamini msanii mchanga akapata nafasi moja akawa ndo mbeba stori na ukamtambulisha moja kwa moja kwenye jamii, utakuwa umezalisha vipaji vipya na kukuza sanaa yetu.”

Habari Zifananazo

Back to top button