Tulia Street Talent yafana

ZAIDI ya TZS Milioni 10 zimetolewa kama zawadi kwa washindi wa msimu wa nne (4) wa mashindano ya vipaji maarufu ‘Tulia Street Talent Competition’ ambayo walihusisha washiriki zaidi ya 200.

Mashindano hayo yaliyodumu kwa siku tatu (3) kuanzia Novemba 17 -19 yalihusisha vipengele tofauti ikiwa ni pamoja na uchekeshaji, mitindo, uimbaji na dancers ambapo jopo la majaji likiongozwa na Kipepeo Mweusi, Mwasiti walifanya kazi kubwa ya kuwapata washindi walioondoka na zawadi hizo tajwa.

Licha ya kuwashindanisha, washiri/wasanii hao walipata semina kuhusu mambo mbalimbali ya sanaa iliyowezeshwa na Mwasiti.

Advertisement

Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya Tulia Trust ya Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU),Tulia Ackson.

Tazama orodha ya washindi wa jumla pamoja na kitita walichojipatia;

MITINDO – WANAUME

1.Denis Shaku – Sh1,000,000/=
2.Isack Lwitiko –  Sh 700,000/=
3.Fadhili Mtweve – Sh 500,000/=

MITINDO – WANAWAKE

1.Justina Jackson – Sh 1,000,000/=
2.Moureen John – Sh 700,000/=
3.Doreen Melckzedek -Sh 500,000/=

DANCERS (Makundi)

1.Swax Dancers – Sh 2,000,000/=
2.Waarabu Dancers – Sh1,500,000/=
3.The Real Kings Dancers – Sh1,000,000/=

COMEDY/UCHEKESHAJI

1. Musa Piliton- Sh1,000,000/=
2.Eliah Mbilinyi –  Sh 700,000/=
3.Jebon Patrick –  Sh 500,000/=

 

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *