Tume ya Tehama, Unesco wasaini kufanya utafiti

TUME ya TEHAMA Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Elimu,Sayansi, na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), imesaini makubaliano ya kufanya utafiti nchini kuhusu upatikanaji na matumizi ya intaneti lengo likiwa ni kuona ujumuishi wake katika masuala mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume, Dk Nkundwe Mwasaga amesaini makubaliano hayo leo Dar es Salaam na Mkuu wa UNESCO, Tanzania Michel Toto.

Akizungumza Dk Mwasaga amesema utafiti huo utafanyika kwa miezi mitatu kuanzia sasa ambapo watazunguka kwenye mikoa kadhaa, ili kupata taarifa za intaneti na kwamba ni watu gani wanaotumia na wanatumiaje.

Amesema kwa UNESCO wanaamini kuwa inteneti ni huduma ya watu wote na katika utafiti huo wanataka kujua Tanzania imefikia hali hiyo na kama bado kufahamu nini kifanyike ili iwe huduma ya watu wote.

” Kwa kufanya hivyo itasaidia sera kutengenezwa vizuri, kwa sasa intaneti sio anasa bali inatakiwa itumike maeneo mbalimbali na Tanzania iweze kwenda kwa kasi zaidi,” amesema Mwasaga na kuongeza kuwa tume hiyo inalenga ifikapo mwaka 2025 watumiaji wa intaneti wafikie ailimia 80.

Amesema utafiti kama huo ulitakiwa ufanyike muda mrefu na UNESCO ina viashiria zaidi ya 100 na utawezesha kuona kama huduma hiyo ni jumuishi na kama haipo kama inavyotakiwa jumuiya za mataifa ziweze kujua wapi pa kusaidia.

Habari Zifananazo

Back to top button