Tume yabariki watuhumiwa walioachiwa kukamatwa

TUME ya kuangalia namna ya kuboresha taasisi za hakijinai imependekeza utaratibu wa watuhumiwa kukamatwa baada ya kufutiwa mashitaka uendelee.

Muhtasari wa ripoti ya tume hiyo unasema ni muhimu utaratibu huo uendelee  kutokana na umuhimu wake katika kulinda maslahi ya umma kwa kumwezesha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kufuta mashauri ambayo yamekosa uhalali wa kuwepo mahakamani wakati uamuzi huo unafikiwa.

Tume imependekeza elimu itolewe kwa wadau wa haki jinai kuhusu maboresho ya mfumo wa watuhumiwa kukamatwa baada ya kuachiwa ,yaliyofanyika kutokana na marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai yaliyofanyika na kuweka sharti kuwa, mashauri yasifunguliwe pasipokuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwasilisha mahakamani na kuendelea na usikilizwaji.

Muhtasari huo pia umependekeza marekebisho yaliyofanyika yakishindwa kutatua changamoto za matumizi ya mamlaka ya watuhumiwa kukamatwa baada ya kuachiwa  marekebisho zaidi yafanyike ili utaratibu huo uwe inatolewa kwa ridhaa ya mahakama.

Tume hiyo pia imependekeza maofisa wa mahakama na waendesha mashtaka watakaoshindwa kuzingatia matakwa ya sheria chini ya kifungu cha 91(3) cha CPA wachukuliwe hatua za kinidhamu na mamlaka zao za ajira.

Alieleza kuwa ilipokea malalamiko ya wadau kuhusu matumizi ya kukamata watuhumiwa baada ya kuachiwa kwamba baadhi ya watuhumiwa waliofutiwa mashtaka hukamatwa tena na kushtakiwa kwa makosa sawa na yaliyofutwa.

Tume ilieleza kuwa Tume ya Mapitio ya Mfumo wa Mahakama ya Mwaka 1977 maarufu kama Tume ya Msekwa ilieleza dhahiri kuwa utaratibu wa kukamata watuhumiwa baada ya kuachiwa haumalizi shauri hivyo mtuhumiwa anaweza kukamatwa na kushtakiwa tena kwa kosa sawa na lile alilofutiwa.

“Aidha, ili kulinda haki ya mtuhumiwa, zimefanyika jitihada mbalimbali za kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka ya kukamata watuhumiwa baada ya kuachiwa nchini. Mathalan, mwaka 2022 kifungu cha 91(3) cha CPA kiliongezwa ili kuzuia mtuhumiwa kukamatwa na kushtakiwa tena ikiwa upelelezi haujakamilika,”ulieleza muhtasari wa ripoti hiyo.

Ulieleza kuwa tume imebaini kuwa, hakuna uelewa wa kuridhisha kuhusu matumizi ya kifungu cha 91(3) cha CPA kinachoweka sharti kuwa mtuhumiwa akishtakiwa tena baada ya kufutiwa kosa ni sharti pawepo ushahidi wa kutosha na usikilizaji wa shauri uanze siku hiyo ya kusomewa shauri upya.

Habari Zifananazo

Back to top button