KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Michael amesema serikali imejipanga kikamilifu kutumia mifumo ya Tehama ili kukabiliana na ushindani wa ukuaji wa mifumo ya ubunifu na teknolojia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kongamano la siku mbili la uvumbuzi lililoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema uvumbuzi utasaidia nchi kwa Maendeleo endelevu.
“Kipindi hiki ni cha Tehama wizara tumewekeza kwa masuala hayo na serikali inazingatia masuala ya tehama kujenga ubunifu wa Watanzania tunazingatia katika mitaala kuanzia shule za masingi,” amesema.
Katibu Mkuu huyo amesema licha ya kongamono hilo,ubalozi wa Japan kupitia JICA wamekuja chuo kikuu cha Dar es Salaam kuadhimisha miaka 60 ya JICA na maendeleo ya nchi zote mbili.
“Leo tumekutana kufanya majadiliano ya ubunifu ya maendeleo endelevu wa nchi zote mbili, ubunifu kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na Japan na hili litasaidia kubadilisha uzoefu,kupata mawazo mapya na kutumia uvumbuzi kwa maendeleo endelevu,”amesema Michael.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa UDSM, Prof Boniventure Rutinya, amesema lengo ni uanzishwaji wa programu hiyo ni kujifunza kutoka Japan kutokana na nchi hiyo kuendelea bila kupoteza utamaduni wao na kufata umagharibi.
Amesema Japan imepiga hatua katika Tehama na kukua kwa tekonolojia hivyo watashirikina nao katika ubunifu na teknolojia.
“Tuna majukumu ya kufundisha, kutafiti na kubadilisha maarifa huko nyuma hatukuwekeza kwenye ubunifu, tulikuwa hatutoki nje ila sasa tunataka kuungana na sekta husika na sio vya ndani tu hata katika sekta ya kijamii,” amesema.
Naye balozi wa Japan Nchini Tanzania Yusushi Misawa amesema Tanzania inatarajia kuwa ya uchumi wa juu miaka ijayo ,hivyo jitihada hizi ni mihumu.
Amesema Japana kupitia JICA inafadhili masomo kwa wanafunzi wa kitanzania na ushirikiano huo utaendelea.
Mwakilishi wa JICA, Yamamura Naofuma alisema kongamano hilo litawaleta pamoja wanataalamu wa Tanzania na Japani kubadilishana uelewa na uzoefu katika masuala ya uvumbuzi kupitia majadiliano