‘Tumieni fursa Chuo cha Mwalimu Nyerere’

TAASISI za serikali na binafsi pamoja na vyama vya siasa vimetakiwa kutumia fursa iliyopo Chuo cha Mwalimu Nyerere ya kukuza ubunifu na teknolojia, ili ziweze kujenga uwezo wa kuzalisha viongozi mahiri.

Rai hiyo imetolewa na  Naibu Katibu Mkuu Wizara aa Elimu, Sayansi Na Teknolojiam Dk Franklin Rwezimula katika kongamano la kumbukumbu ya kuzaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere  iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema ni vyema wakatumia teknolojia zilizopo katika chuo hicho, kwani zitasaidia kuboresha kizazi cha sasa hasusani kukuza elimu katika viwango vya juu zaidi.

Akizungumzia uboreshaji wa maendeleo nchini, Rwezimula amewataka Watanzania, vyama vya siasa pamoja na viongozi wa dini  kuunga jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kusimamia mambo mbalimbali katika jamii, lengo ni kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya chuo, Stephen Wasira amesema Hayati  Mwalimu Nyerere, amefanya kazi kubwa na ameacha misingi mingi ya umoja na mshikamano, bila kujali kabila wala dini, hivyo Watanzania wazidi kuienzi, kwani kwa kufanya hivyo watadumisha uzalendo.

Habari Zifananazo

Back to top button