MKUU wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amewataka wananchi watumie simu kuwasiliana na makarani wa sensa endapo itatokea majukumu yao yakasababisha washindwe kuwasubiri majumbani.
Alisema hayo jumatano baada ya kutembelea Wilaya ya Kilolo kuona maendeleo ya shughuli hiyo ya kuhesabu watu.
Karani wa Kitongoji cha Ilala A katika Kijiji cha Lulanzi, Wito James alisema: “Kuna kaya mbili tofauti zilinipigia simu nifike nyumbani kwao kabla ya saa moja asubuhi kwa ajili ya kuhesabiwa kwani baada ya muda huo zisingekuwepo nyumbani na nikafanya hivyo.”
James alisema shughuli hiyo inakwenda vizuri na wananchi wanatoa ushirikiano mzuri na mpaka ilipofika saa tano mchana jana alikuwa ameshakutana na kaya 14 na nyingi kati ya kaya hizo zina watu zaidi ya watano.
Dendego aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaotoa akisema hakuna mwananchi atakayeachwa bila kuhesabiwa