‘Tunairejesha Tanga ya viwanda’

Serikali mkoani Tanga, imesema kuwa itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kwenye fursa za viwanda, ili kuirejesha Tanga ya viwanda.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha kadi za kieletroniki (smart card) cha Rubash Investment kilichopo jijini Tanga.

Amesema mkoa huo umeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, ili kuchangia ukuwaji wa uchumi na kutekeleza agenda ya serikali ya awamu ya sita ya uchumi wa viwanda.

“Tumeweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuvutia wawekezaji na Moja ya uwekezaji mkubwa ni uwepo wa kiwanda hiki kikubwa ambacho kwa Afrika kinapatikana hapa Tanga pekee,”amesema RC Mgumba.

Kwa upande wake mwekezaji wa kiwanda hicho Rashid Liemba, ameiomba serikali kuwapa tenda ya kutengeneza vitambulisho sambamba na kadi mbalimbali.

“Kiwanda hiki ni mbadala wa kupunguza gharama za kutengeneza smart card nje ya nchi, tunachoomba serikali na taasisi nyingine ziweze kutuletea mahitaji yao hapa tuweze kutengeneza vitambulisho, “amesema Liemba.

Habari Zifananazo

Back to top button