‘Tunaomba nasi tuhamie Msomera’

“Tunaiomba serikali ifanye hima kutuondoa huku, maana hivi sasa tumetengwa na wenzetu, hakuna uzalishaji mali tunaofanya tulichukua hela zetu kwenye vicoba vyetu tukidhani tunaondoka mapema sasa hela zimeisha tumebaki tukisubiri serikali ituondoe, tukiwa Msomera tutacheza vicoba vyetu kwa amani na kujikwamua kiuchumi”.

Hizo ni sauti za wanawake na familia zao zenye kaya zaidi ya 50 zinazoiomba serikali kuwaondoa eneo hilo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Wanawake hao wakiongozwa na Elizabeth Makamero na Juliana Laltaika wanaocheza vicoba ili wajikwamue kiuchumi kwa kuanzisha biashara za aina mbalimbali ikiwemo mifugo kutoka kata ya Nainokanoka ndani ya hifadhi hiyo, wanaomba serikali kuwahamisha ili waende Msomera kwenye uhuru zaidi ya hapo.

Makero anasema kinamama wanapata changamoto mbalimbali zikiwemo kutofanya shughuli za maendeleo, ikiwemo kucheza vicoba vinavyowasaidia kukopa fedha.

Anasema baadhi ya wanawake waliokuwa wakicheza vicoba wamejiondoa na kupewa fedha zao tangu mwaka jana wakati wanasubiri kuondoka, lakini hadi leo bado hawajaondoka na kushindwa kufanya shughuli zao za awali zikiwemo biashara ndogondogo na nyinginezo za kuhudumia familia.

Juliana Laltaika akiwa na mume wake Thadei Saitoti Laizer anasema kuwa wanashindwa kujitafutia shughuli nyingine kwa sabababu wanasubiri kuhamia Msomera, hivyo ni vyema sasa serikali ikawahamisha waliokubali kuondoka eneo hilo, ili wakaanze maisha mapya yenye huduma mbalimbali za kijamii.

Habari Zifananazo

Back to top button