‘Tunarudi Tanzania tukiwa mashujaa’
AFRIKA KUSINI: Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema anajivunia kile kilichofanywa na timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kutupwa nje kwenye michuano hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Burkinafaso amesema wachezaji pamoja na viongozi walifanya kila kitu kwa ajili ya mafanikio ya timu hiyo jambo lililokaribia kukamilika lakini isivyo bahati ndoto zao hazikutimia.
Ameongeza wanarudi Tanzania wakiwa mashujaa lakini wakiwa na mengi waliyojifunza kwenye michuano hiyo.
Aidha akijibu maoni ya moja ya shabiki wa timu hiyo aliyemuomba asiondoke kikosini hapo mchezaji huyo amesema atasalia ndani ya timu hiyo ili kutimiza malengo ya timu.