‘Nasimama na Samia’

LOLIONDO, Arusha: WAZIRI wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema athari za kazi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika nyanja ya biashara, elimu, siasa na sekta mbalimbali nchini zinatosha kuueleza ulimwengu namna wananchi wanajivunia serikali yao.

Hayo ameyasema leo Aprili 15,2024 wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa vituo vya kurushia matangazo ya Redio TBC Taifa na Bongo Fm

Advertisement

Nape, amevitaka vyombo vya habari vilivyofunguliwa na Rais Samia wasimame kwa pamoja na kueleza kazi nzuri zinazofanywa na kiongozi huyo duniani kote hasa katika sekta ya habari

“Wanahabari wenzangu ambao vyombo vyao vilifungiwa,walikuwa wanafanya kazi kwa hofu, mitandao iliyofunguliwa twendeni leo tukaiyambie dunia tunasimama na mama,” amesema Nnauye

Pia, ametoa wito kwa wote wanaoguswa na kazi za Rais Samia mitandaoni kuanzia sasa waiambie dunia wanasimama na Rais Samia kwa mambo mema yote anayoyafanya kupitia #TunasimamaNaSamia.