Tunda Man: Sitozi pesa wasanii wanaonishirikisha

Msanii wa Bongo Fleva ,Khalid Ramadhan maarufu Tunda Man amesema hatozi gharama yeyote kwa wasanii wanaomshirikisha katika nyimbo zao kwa sababu anaamini katika kukuza vipaji vya wasanii wanaochipukia.

Msanii huyo amesema anaamini katika kusaidia ndiyo maana hatozi gharama yeyote kwa msanii anayemshirikisha katika wimbo wake akiamini kila msanii ana nyota yake katika muziki anaofanya.

Tunda Man anaongeza kwamba licha ya kukubali kushirikishwa na msanii yeyote mwenye jina ama asiye na jina lakini huwa anachagua sana anapotaka kumshirikisha msanii kwenye wimbo wake.

“Mimi naamini katika kipaji cha msanii na sitozi mtu pesa yoyote anaponishirikisha katika wimbo wake lakini ninapotaka kumshirikisha msanii katika wimbo wangu lazima awe anajua kuimba kweli, ukiangalia wasanii wote niliowashirikisha katika nyimbo zangu wanajua kuimba,” alisema Tunda Man.

Tundaman kwa sasa anatamba na wimbo wa singeli unaoitwa ‘Nakuposti’ alioimba na Balaa Mc anasema wasanii wote aliowashirikisha katika nyimbo zake wana uwezo wa kuimba lakini pia wanaujua muziki.

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button