Tundu Lissu: Nimefurahi kurudi nyumbani

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema amefurahi kurudi nyumbani Tanzania leo Januari 25, 2023, baada ya kuishi kwa muda mrefu nje ya nchi.

Akihutubia wananchi viwanja vya Bulyiga, Temeke Dar es Salaam, amesema kuishi nje ilikuwa kipindi kigumu sana kwake.

Amezungumza mambo mbalimbali ikiwemo suala la Katiba, ambalo alisema kwa upande wake ni jambo la umuhimu la kufanyiwa kazi.

Habari Zifananazo

Back to top button