HAIKUWA kazi nyepesi kutimiza kile walichokuwa wakikihitaji, huenda walitaka kuvunja ile historia yao mbovu inayowandama, Tunisia imeondolewa katika Mashindano ya Kombe la Dunia, licha ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa.
Ushindi wa bao 1-0 wa Australia dhidi ya Denmark umeiondoa Tunisia na kuifanya timu hiyo iendelee kuwa na rekodi ya kutovuka katika hatua ya makundi tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1930 nchini Uruguay.
Bao hilo limefungwa na Wahbi Kazri Katika kundi D, Ufaransa imemaliza ikiwa na pointi sita sawa na Australia, wakati Tunisia imemaliza ikiwa nafasi ya tatu na pointi nne, Denmark wamevuna pointi moja pekee.
Tangu mwaka 1930, Tunisia haikuwahi kushiriki mpaka ilipofika mwaka 1978 na kuishia makundi. kuanzia 1982 haikufuzu tena hadi 1998, 2002 na 2006 ambapo pia iliishia makundi.
Mwaka 2010, 2014 haikufuzu, 2018 ilifuzu na kutoka hatua ya makundi tena. Leo inacheza na Ufaransa, na sasa anaondolewa tena.