Tunisia itaifunga Ufaransa?

Tangu mwaka 1930, lilipoanzishwa Kombe la Dunia, Tunisia haikuwahi kushiriki mpaka ilipofika mwaka 1978 na kuishia makundi. kuanzia 1982 haikufuzu tena hadi 1998, 2002 na 2006 ambapo pia iliishia makundi.

Mwaka 2010, 2014 haikufuzu, 2018 ilifuzu na kutoka hatua ya makundi tena. Leo inacheza na Ufaransa, swali atashinda?

akifungwa hayupo.

Kwa historia hiyo maana yake ni kuwa timu hiyo haijawahi kupita hatua ya makundi kwenda 16 bora kwa miaka aliyoshiriki mashindano ya Kombe la Dunia.

Michezo minne ya Kundi C na D ya michuano ya hiyo itapigwa leo, michezo hiyo inakamilisha ratiba ya makundi, matumaini ya Tunisia kufuzu madogo sana, kwani wana pointi moja na wanamaliza na Ufaransa saa 12:00 jioni.

Kundi D, Ufaransa amefuzu, Australia ana pointi tatu, Denmark na Tunisia wana moja.

Ili Tunisia afuzu na kuungana na Senegal kwa timu za Afrika, anatakiwa kuifunga Ufaransa kisha aombe sare ya bila kufungana Australia na Denmark, ili kuondoa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga dhidi ya Australia.

Michezo mingine ya kundi C, Poland wenye pointi nne, anacheza na Argentina mwenye tatu, Mexico mwenye moja na Saudi Arabia mwenye tatu.

Endapo Saudi Arabia itaifunga Mexico, watafikisha pointi sita, kwa mantiki hiyo itaungana na mshindi kati ya Poland na Argentina.

Habari Zifananazo

Back to top button