Tutaenda kuiduwaza Yanga-Masau Bwire

TIMU ya soka ya Ruvu Shooting, imetamba kuwa itaenda kuiduwaza Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika leo usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, kwenye mahafali ya shule ya Msingi Blessed Hill, iliyopo Kitunda Dar es Salaam, ambapo Bwire alikuwa mgeni rasmi.

“Nimekuja kwa shughuli ya mahafali ya Blessed Hill, lakini si vibaya nikatoa pia salamu zangu hapa kwamba Yanga haijapoteza mechi ya ligi kwa muda mrefu, naomba tukutane Uwanja wa Mkapa kesho (leo), tunaenda kuwaduwaza,” alisema Bwire na kushangiliwa na wanafunzi, wazazi, walimu pamoja na wageni mbalimbali.

Bwire ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Makumbusho, Dar es Salaam, aliwataka wanafunzi 202 wa Blessed Hill, wanaohitimu darasa la saba, wasiogope kuonesha vipaji vyao, kwani michezo na sanaa hivi sasa ni ajira hapa nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button