‘Tutaendelea kuelimisha kanuni mpya ya kikokotoo’

SERIKALI imesema inaendelea na mpango wa kuwaelimisha wananchi hususani waajiri na wanachama wa Mifuko ya Pensheni wakiwemo wastaafu kuhusu faida ya Kanuni mpya ya mafao ya pensheni.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi alipokua akijibu swali la Mbunge wa Moshi Mjini Priscus Tarimo aliyetaka kujua serikali ina mpango gani kuhusu malalamiko ya wastaafu juu ya kikokotoo kinachotumika kupiga mahesabu na kulipa mafao.

“ Serikali kupitia Mifuko ya Pensheni na kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) imejipanga na inaendelea kutoa elimu ya kanuni hiyo.

“Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2023, Mifuko iliweza kutoa elimu kwa jumla ya waajiri 5,580 (PSSSF 362 na NSSF 5,218) kati ya waajiri 6,200 waliopangwa kufikiwa kipindi hicho.

“Aidha, wanachama 131,497 (PSSSF 35,133 na NSSF 96,364) walifikiwa na mafunzo hayo.

Mifuko inaendelea kutoa elimu kama sehemu ya majukumu yao ya kila siku,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button