Tutaleta Umeme hata kama Nyumba ya nyasi

GEITA; Bukombe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema shauku ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona kila Mtanzania anapata umeme bila kujali aina ya nyumba aliyonayo, kwani kila Mtanzania anahitaji mwanga.

Dk Biteko amesema hayo leo Septemba 26, 2023 wakati wa hafla ya uwashaji umeme kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili katika Kijiji cha Ihako kilichopo Kata ya Katome, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

“Tutaleta umeme vijijini, hata kama wananchi hawana nyumba nzuri wanahitaji mwanga, hata kama wana nyumba za nyasi ambazo hazina tarazo wanahitaji mwanga. Watakapopata umeme watapata shauku ya kujenga nyumba nzuri,” amesema Dk Biteko.

Amesema serikali imeanza kusambaza umeme katika ngazi ya vijiji na baada ya vijiji vyote kupata umeme itashuka katika vitongoji.

Ameiagiza REA kwenda vijijini na kuzungumza na wananchi ili kujua changamoto zao na kuzitatua.

“Nendeni kwa wananchi, nendeni vijijini zungumzeni na wanavijiji, tukaongee lugha zao, tunataka kuona shughuli za REA zikifanyika vijijini na sio mjini, kazi kubwa ya REA ni kupeleka umeme vijijini na sio mijini, hivyo tunataka kuwaona kazi zenu mkifanyia vijijini,” amesema Dk Biteko.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unalenga kupeleka umeme katika vijiji vyote ambavyo awali havikuwa na umeme, ambapo katika Mkoa wa Geita vijiji 62 na vitongoji vikubwa 65 vitapatiwa umeme kupitia mradi huo, hivyo kufanya jumla ya vijiji/vitongoji vitakavyopatiwa umeme kupitia mradi huu kuwa 127.

“Mkoa wa Geita una jumla ya vijiji 461 ambapo vijiji 399 sawa na asilimia 86.6 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali ikiwemo REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza.

“Wakala wa Nishati vijijini umeendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Geita ikiwa na lengo la kuwapatia huduma za Nishati kwa wananchi ili kuboresha huduma za jamii na kuimarisha shughuli za kiuchumi,” amesema Mhandisi huyo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback
2 months ago

[…] post Tutaleta Umeme hata kama Nyumba ya nyasi first appeared on […]

JenniferGale
JenniferGale

I’ve got my first check for a total of 13,000 dollars. I am so energized, this is whenever I first really acquired something. I will work much harder now and I can hardly hang tight for the following week installment.
.
.
Detail Here…………………………………………………………….. http://Www.BizWork1.Com

KaliMcDougall
KaliMcDougall

I even have made $17,180 only in 30 days straightforwardly working a few easy tasks through my PC. Just when I have lost my office position, I was so perturbed but at last I’ve found this simple on-line employment & this way I could collect thousands simply from home. Any individual can try this best job and get more money online going this article…..
>>>>>   http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by KaliMcDougall
CharleeJewell
CharleeJewell
2 months ago

[ JOIN US ] I am making a good salary from home $16580-$47065/ Dollors week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. ( y72q) I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………> http://Www.SmartCareer1.com

Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x