Tutunze fasihi-Prof Mkenda

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ili kukuza lugha zetu ni lazima tuendeleze, tutunze na kuenzi fasihi.

Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Februari 20, 2024 jijini Dar es Salaam alipozungumza na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa Kuhusu Dhima ya Lugha za Asili katika kujenga tamaduni – mtambuka,  diplomasia ya kiisimu ya kiuchumi.

Aidha,Prof Mkenda ameongeza kuwa kwa sasa Serikali imeanzisha tuzo ya uandishi bunifu zinazojulikana kama tuzo za Mwalimu Julius Nyerere  zinazotolewa katika maeneo ya hadithi fupi, tamthilia na hadidhi za watoto ambazo zimeanza mwaka 2023.

Ameongeza kuwa hata katika mabadiliko ta mitaala kumeongezwa lugha nyingi zaidi zinazofundishwa kwa hiari zikiwemo Kiarabu, Kifaransa na Kichina ambapo mwanafunzi wa elimu ya msingi anaweza kuchagua kuzisoma na kuwa selikali itaendelea kutafakari zaidi ili kuongeza lugha nyingine na kuhakikidha lugha zinachangia katika diplomasia ya kiisimu kiuchumi.

Habari Zifananazo

Back to top button