Tuzo za MTV EMA 2023 zasitishwa

SHEREHE za ugawaji wa tuzo za muziki MTV EMA zilizopangwa kufanyika Paris, Ufaransa Novemba 5 mwaka huu zimesitishwa.


Kwa mujibu wa Sky News na mitandao mingi ya burudani, hatua hiyo imetokana na sababu za kiusalama, na matukio yanayoendelea duniani ikiwemo vita ya Israel na Palestina.

Katika taarifa yake ya kutangaza uamuzi huo, msemaji wa kampuni ya Paramount inayomiliki MTV alisema: “Kutokana na kuyumba kwa matukio ya dunia, tumeamua kutosonga mbele na MTV EMA 2023 kutokana na tahadhari nyingi kwa maelfu ya wafanyakazi. wahudumu, wasanii, mashabiki na washirika wanaosafiri kutoka kila pembe ya dunia,”

“MTV EMAs ni sherehe ya kila mwaka ya muziki wa kimataifa. Tunapotazama matukio mabaya kama Israeli na Gaza yanaendelea kutokea, hii haihisi kama wakati wa sherehe ya kimataifa. Huku maelfu ya maisha tayari yamepotea, ni wakati wa maombolezo.” alieleza.

Taylor Swift, Olivia Rodrigo, Miley Cyrus na Nicki Minaj ni miongoni mwa wateule wa ngazi za juu katika tuzo hizo.

Imeelezwa zoezi la upigaji kura linaendelea na washindi watapatiwa tuzo zao

Habari Zifananazo

Back to top button