Twaha Kiduku: Simuwazii Mwakinyo

BONDIA Twaha  Kassim maarufu ‘Twaha Kiduku’ amesema kwa sasa hana wazo la kupambana na bondia, Hassan Mwakinyo badala yake anaangalia mambo yake mengine pamoja na mapambano yake yaliyoko mbeleni.

Kiduku anatarajiwa kupanda ulingoni Desemba 26, 2023 katika Ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo anatarajiwa kupigana na bondia Mohammed Sebyala.

“Sumuwazii Mwakinyo kwa sasa nafikiria mambo yangu mengine yakiwemo mapambano yanayonikabili hivi karibuni,” amesema Twaha Kiduku.

Kiduku ameongeza kwamba yeye hana tabia ya kuchagua bondia wa kupigana naye kinachotakiwa ni rekodi ya bondia huyo iwe ya kumpeleka mbele.

“Mi na timu yangu hatuchagui bondia tunaangalia rekodi ya bondia anayetaka kupigana nasi tunamkaribisha huyo bondia mwingine hata simfikirii,” amesema Kiduku.

Kiduku baada ya kupoteza mchezo wake wa mwisho na bondia kutoka Misri amesema anakwenda katika pambano lake la Desemba 26 kama nyoka aliyekanyagwa mkia .

Habari Zifananazo

Back to top button